Skip to main content

VYAKULA VINAVYOFAA KWA MTOTO KUANZIA MIEZI SITA MPAKA MIEZI TISA

 



Ni wakati wa kuwa mbunifu sasa! Mtoto wako akiwa na miezi 6 mpaka 9 anakua na hamu ya kujaribu chakula kipya, na pengine kuanza kujifunza kutafuna pia. Sasa unahitaji kujifunza jinsi ya kuandaa milo ambayo itamvutia na kumshawishi mtoto kula vizuri. 
 
JEE VYAKULA GANI NI VIZURI KUMWANZISHIA MTOTO MWENYE UMRI WA MIEZI SITA MPAKA TISA?
 
Wazazi na walezi wengi huuliza suali hili kwa lengo la kuhakikisha watoto wao wanapata chakula bora zaidi. Hakuna sheria wala kanuni katika suala hii. Watoto wote wako tofauti, kwa tabia zao maalumu za kupenda na kukataa vitu.
Taarifa na mapishi yaliyomo kwenye sehemu hii ni mwongozo tu, kama mtoto wako hatopenda basi mwache kama wiki hivi halafu jaribu kumpa tena. Ladha kwake hubadilika kila mara kutokana na ukuaji wake wa haraka, hivyo kitu ambacho amekipenda leo huweza baada ya wiki akaanza kukikataa, na kinyume chake pia ni sawa.
NB: kumbuka kutumia kanuni ya siku nnee kila unapomuanzishia mtoto chakula kipya (yani kumpa mtoto chakula angalau ndani ya siku nne kabla hujambadilishia na kumpa kingine) . Hii husaidia kujua vyakula ambavyo vinamletea mtoto mzio.
 
MATUNDA NA MBOGA MBOGA
Mara baada ya mtoto wako kufurahia vyema rojorojo za matunda na mboga mboga, unaweza kuanza kumchanganyia ladha ya vyakula vingine vichache na kuongeza uzito wa milo yake.
 
NYAMA
Nyama ni chanzo kizuri cha protini, lakini katika kipindi hiki mtoto hupata protini kutoka kwenye maziwa.
Sababu kubwa ya kuweka nyama kwenye vyakula vya watoto ni kwa ajili ya kumpatia madini chuma ya ziada. Hii ni kwasababu hifadhi ya madini chuma ya mtoto inaweza kuanza kuisha anapofikisha umri wa miezi sita hadi tisa.
Madini chuma ni muhimu sana katika damu, husambaza oksijini kwenye tishu/seli za mwili na kutoa nguvu inayohitajika kwa ajili ya ukuaji.
Katika makala za hapo mbele tutaelezea ni muda gani muafaka wa kumpa mtoto wako nyama. Nyama ya kuku au bata mzinga ni nzuri sana kumwanzishia mtoto. Ukihitaji kujifunza zaidi mapishi ya aina mbali mbali ya chakula cha watoto kuanzia miezi saba ambayo yamechanganywa na kuku fatilia zaidi mada zetu kwenye group maalumu la Whatsapp ambalo ukijiunga utafundishwa jinsi ya kuandaa milo hiyo. Pia utapata kitabu chenye aina mbali mbali za mapishi ya watoto kuanzia miezi sita hadi miezi ishirini na nne.
Usimpe mtoto nyama za makopo kwani mara nyingi huwa na chumvi nyingi sana na hazina virutubishi vya kutosha kukidhi mahitaji ya kila siku ya mtoto.
Mtoto anapokua amezoea nyama ya kuku na bata mzinga, basi unaweza sasa kumuanzishia nyama ya ng’ombe au mbuzi. Tutawaletea mapishi mbali mbali ya nyama ili muweze kujaribu.
 
SAMAKI
Samaki wana protini nyingi sana, pamoja na madini ya potasiam na vitamin. Kwa hiyo samaki ni chakula bora na chenye afya zaidi kwa mtoto.
Pia samaki wana fatty acid aina ya omega 3, ambayo ni muhimu sana kwa afya ya ubongo na kujenga uelewa mzuri kwa mtoto. Pia husaidia katika kuondoa mafuta mabaya mwilini hivyo kukinga na magonjwa ya moyo ikiwemo shinikizo la juu la damu.
Kuna aina kadhaa za mapishi ya kuchanganya na samaki, ambayo unaweza kumwanzishia mtoto wa miezi saba. 
 
MTINDI
Mtindi ni salama kwa mtoto kuanzia miezi sita, lakini ni vizuri kutumia mtindi wa asili ambao haujaongezwa sukari. Tumeweka maelezo jinsi ya kuandaa mtindi wewe mwenyewe nyumbani kwa ajili ya mtoto na familia yako kwa jumla. Unaweza kuongeza matunda kumvutia zaidi mtoto lakini usiweke sukari wala asali hata kidogo. Usimpe mtoto asali katika umri wa chini ya mwaka mmoja kama tulivyoeleza kwenye sehemu ya vyakula vya kuepuka kumpa mtoto chini ya mwaka mmoja.
 
CHEESE/JIBINI
Unaweza kuana kumpa mtoto wako wa miezi sita mpaka tisa jibini, ingawa baadhi ya jibini watoto wengi hawazipendi. Tafuta ambayo ina ladha nzuri. Kuna mapishi kadhaa ambayo unaweza kuweka jibini kama tutakavyowaletea kwenye sehemu ya maelezo ya mapishi mbali mbali.
 
MAYAI
Kumuanzishia mtoto vyakula vilivyowekwa kiini cha yai hakuna tatizo lolote. Lakini vizuri kufatilia kwa umakini unapoanza kumpa mtoto yai lote kwani ile sehemu nyeupe huleta mzio kwa baadhi ya watoto.
Kiini cha yai hufanya rojorojo ya chakula cha mtoto kuwa na uzito mzuri hasa kama umetokea kuwa laini sana. Kiini cha yai pia husaidia kukuza ubongo wa mtoto wako, kwa hiyo mara kwa mara changanya kiini cha yai kwenye milo ya mtoto wako ili kusaidia kuimarisha lishe yake. 
 
VYAKULA JAMII YA KUNDE
Hivi ni vyakula kama maharage, kunde, mbaazi, dengu n.k. ni vyakula vyenye protini nyingi, vitamin na madini kwa hiyo ni vizuri kuchanganya kwenye milo ya mtoto.
Hata hivyo unatakiwa kuwa na tahadhari! Tunatambua vyakula hivi husababisha gesi kwa hiyo usimpe mtoto mara kwa mara aina hii ya vyakula.
Kwa mapishi yanayojumuisha vyakula vya kundi hili kwa watoto wa umri wa miezi sita hadi tisa fatilia masomo yetu zaidi na pia pata nakala yako ya kitabu cha mapishi ya vyakula vya nyongeza kwa watoto wa umri wa miezi sita hadi ishirini na nne.

Comments

Popular posts from this blog

MAPISHI YA MISHIKAKI LAINI NA MITAMU SANA (JUICY MISHIKAKI)

Jinsi ya kupika mishkaki MAHITAJI 1.Nyama nusu kilo 2.Vitunguu saum vilivyosagwa kijiko kimoja cha chai 3.Tangawizi iliyosagwa kijiko kimoja cha chai 4.Mafuta ya kupikia vijiko viwili vya chakula 5.Pilipili manga kijiko kimoja cha chai 6.Juisi ya limao nusu kikombe 7.Pilipili ya unga nyekundu kijiko kimoja cha chai 8.Tandoori masala au beef masala nusu kijiko cha chai 9.Vipande vya hoho vya shepu ya box 10.Vipande vya karoti vya shepu ya duara.   MAPISHI 1.Katakata nyama yako katika vipande vipande vidogo vya mishikaki 2.Chukua bakuli kubwa kisha mimina vitunguu saum,tangawizi,pilipilimanga,pilipili ya unga,tandoori masala kisha kamulia limao au ndimu kisha changanya vizuri. 3.Mimina vipande vya nyama katika hilo bakuli kisha changanya vizuri 4.Funika bakuli lako na acha kwa muda wa saa 1 hadi 3 au hifadhi kwenye fridge usiku kucha katika ubaridi wa wastani. 5.Loweka vijiti vya mishikaki katika maji kwa dakika 10. 6.Funua bakuli lako kisha chukua vijiti vya mishikaki kisha anza kuc...

MAPISHI YA TAMBI ZA BOMBA NA NYAMA YA KUSAGA

 Leo nitawaelezea jinsi ya kupika tambi tamu sana pamoja na nyama ya kusaga. Tambi zetu za leo ni tambiza bomba. Naam, Mapishi ya tambi yapo ya aina tofauti tofauti, kuanzia tambi za sukari na za chumvi ambazo kwamba aghlabu huandaliwa kwa nyama ya kusaga. Hata hivyo, wapo wengine wanaoandaa tambi kwa mchuzi wa viazi au hata mayai. Na leo nitawaelezea jinsi ya kupika tambi tamu sana za bomba pamoja na nyama ya kusaga.     MAHITAJI   1.Nyama ya kusaga robo kilo 2.Tambi za bomba robo kilo 3.Kitunguu maji kimoja cha wastani (kikate vipande vidogo dogo sana) 4.Nyanya kubwa 2 5.Kitunguu saum kijiko kimoja cha chakula 6.Tangawizi kijiko kimoja cha chakula 7.Pilipili manga ya unga kijiko kimoja cha chai 8.Tomato paste vijiko vitatu vya chakula 9.Chumvi kiasi   MAPISHI   1.Chukua sufuria weka jikoni kisha mimina mafuta ya kupikia 2.Mimina vipande vidogo dogo vya kitunguu maji kisha koroga vizuri 3.Mimina pilipili manga na koroga vizuri 4.Mimina kitunguu saum na ...