Skip to main content

USAFI WA MIGUU

USAFI WA MIGUU:
 
Huu ni Usafi wa miguu ambao hautoi tu sumu mwilini mwako lakini utafanya miguu ipumzike, itandoa harufu mbaya ya miguu baada ya kukaa sana viatu na itaua kabisa bakteria mbaya na fungi mwilini.

 
MAHITAJI:
 
1. Beseni la kuoshea miguu lililojazwa maji ya uvuguvugu
 
2. Kijiko 1 kidogo cha maji ya limao
 
3. Kijiko 1 kidogo cha chumvi ya Epsom au baking Soda (Chochote kitakachopatikana)
 
4. ½ Kijiko cha mafuta ya mzaituni (olive)
 
5. Majani mawili au matatu ya muarubaini
 
6. Scrub ya miguu
 
7. Cream ya miguu yoyote inayopatikana au unaweza kutumia cream ya mwili pia.
 
JINSI YA KUANDAA:
 
Weka vitu vyote vilivyoainishwa (2-5) kwenye bakuli la maji ya moto. Hakikisha kuwa maji yana vuguvugu wa kutosha lakini hayapaswi kuwa moto sana yataunguza ngozi.
Loweka miguu yako katika bakuli kwa dakika 15. Sugua miguu kidogo na scrub ya miguu kisha kausha na kitambaa. Paka moisturizer yako na uende kulala.
Fanya hivi mara kwa mara kadri uwezavyo. Angalau mara moja kila baada ya wiki mbili.
Haitakupa tu utulivu wa mwili wako na akili lakini inapunguza mawazo na hufanya kazi ya kutoa sumu kabisa mwilini mwako kwa wakati huo huo.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUPIKA MAANDAZI/MAHAMRI LAINI NA MATAMU SANA/how to make maanda...

JINSI YA KUKAANGA MIHOGO LAINI/ CASSAVA RECIPE

NJIA MPYA KUPIKA VIAZI VITAMU/ SWEET POTATO STIR FRY