Ngozi za usoni kama tunavyojua zinatofautiana. Kuna uso mkavu..uso wenye mafuta na uso wa kawaida.
Leo hapa ninawaletea namna ya kutunza uso wa mafuta.
Wengi wenu wanayachukia mafuta usoni.. kweli yanakera lakini pia yana uzuri wake. Uso wenye mafuta haushiki mikunjo haraka kama uso mkavu. Hii ndio faida mojawapo kubwa sana ya uso wa mafuta. Na hizi ndio njia za kutunza uso wenye mafuta.
Wengi wenu wanayachukia mafuta usoni.. kweli yanakera lakini pia yana uzuri wake. Uso wenye mafuta haushiki mikunjo haraka kama uso mkavu. Hii ndio faida mojawapo kubwa sana ya uso wa mafuta. Na hizi ndio njia za kutunza uso wenye mafuta.
1. Uso wenye mafuta lazima kuoshwa na facewash sio sabuni za kawaida. Kuna facewash za kupunguza mafuta usoni. Madukani zinapatikana kwa wingi au supermarkets.
2. Uso wenye mafuta unaoshwa mara 2 au 3 kwa siku. Na pia ukirudi tokea safari yako unaosha uso kwa maji ya baridi na facewash.
3. Uso wa mafuta hautaki maji ya moto kabisa. Maji ya moto ni sumu kwa uso wa mafuta. Inazidisha joto na kuleta chunusi nyingi usoni.
4. Uso wenye mafuta na wenye chunusi nyingi sana.. hautakiwi kufanyiwa scrub. Ukifanya scrub machunusi hupasuka na kutoa maji maji yanayosambaa na kuzalisha chunusi nyingi sana na pia kusababisha mafuta kutoka kwa wingi usoni.
5. Uso wenye mafuta husababisha vipodozi kutodumu kwa muda unaotakiwa. Kabla ya kupaka vipodozi usoni... sugua Uso na shingo kwa barafu baada ya hapo unapaka vipodozi.
6. Njia rahisi ya kupunguza mafuta usoni... pendelea kusugulia ndimu usoni. Ndimu Ina acid na hukata mafuta. Kata ndimu kipande na sugua usoni. Kaa nayo mpaka ikauke kisha nawa na maji ya bomba au ukipenda maji ya baridi ya fridge.
Ndimu ya barafu:
Pia unaweza kukamua ndimu za kutosha na kuchanganya na maji na kugandisha ikawa barafu kisha unasugulia usoni. Huleta unadhifu na kupunguza mafuta usoni. INAONDOA NA MADOA PIA.
7. Uso wenye mafuta hautaki joto. Joto namaanisha lotion au mafuta ya aina yeyote yale.. ukipaka lotion au mafuta usoni ambapo tayari Uso una mafuta.. huleta chunusi kwa wingi sana. Chunusi hizo hua ndogo ndogo au kubwa zenye usaha na huacha alama na mabaka usoni.
8. Kama una safari maalum...basi tangulia siku moja kabla au shinda siku nzima na maji ya ndimu usoni na kabla ya kuanza kupaka vipodozi sugua barafu ya kawaida au ya maji ya ndimu na nawa kwa maji ya bomba au ya baridi kutoka katika fridge kisha paka vipodozi.
Hayo ndio mambo mengi ya kuzingatia kuhusu uso wenye mafuta.
Comments
Post a Comment