Umeshawahi kula mishikaki ya kuku tikka?
Jaribu leo mapishi yake
MAHITAJI
1.Minofu ya kuku ya mapaja au ya kifua isiyo na mifupa kilo moja
2.Tangawizi iliyosagwa kijiko kimoja cha chakula
3.Kitunguu saum kilichosagwa kijiko kimoja cha chakula
4.Unga wa giligilani nusu kijiko cha chakula
5.Pilipili ya unga nusu kijiko cha chai
6.Unga wa mdalasini nusu kijiko cha cha
7.Pilipilimanga nusu kijiko cha chakula
8.Limao moja
9.Manjano kijiko kimoja cha chakula
10.Kitunguu maji kimoja
11.Majani ya giligilani
12.Unga wa binzari nyembamba kijiko kimoja cha chai
13.Mtindi nusu kikombe
14.Chumvi kiasi
15.Mafuta ya kupikia kiasi
MAPISHI
1.Katakata minofu ya kuku ya kifua au mapaja kwa umbo la vibox
2.Chukua bakuli kubwa mimina vipande vya minofu ya kuku
3.Mimina viungo vyote vilivyotajwa na mafuta kiasi kisha changanya vizuri.
4.Chukua vyuma vya mishikaki au vijiti vya mishikaki kisha chomeka vipande vya minofu ya kuku
5.Andaa jiko lako la mkaa na wavu wa kuchomea nyama au kama unatumia oven hakikisha joto lipo katika digrii 240 (Kwa kutumia oven ichome kwa dakika 10, kisha ipake mafuta na choma tena kwa dakika 5)
6.Choma mishikaki ya kuku tikka kwa kuipindua pindua katika moto wa wastani ili usiunguze mishikaki yako kwa muda wa dakika 10.
7.Inyunyuzie au ipake mafuta minofu ya kuku wakati unaichoma
8.Hakikisha nyama zimebadirika rangi na kuwa kahawia
9.Mishikaki ya kuku tikka ipo tayari
Katakata kitunguu maji katika vipande kisha weka juu ya mishikaki yako ili kuipa harufu nzuri au weka majani ya giligilani juu yake
Andaa mchuzi wako na wali au na pilipili yako au chatne na mishikaki hii na juisi baridi kisha jionee tofauti.
Comments
Post a Comment