Skip to main content

MAPISHI YA MISHIKAKI LAINI NA MITAMU SANA (JUICY MISHIKAKI)

Jinsi ya kupika mishkaki

MAHITAJI
1.Nyama nusu kilo
2.Vitunguu saum vilivyosagwa kijiko kimoja cha chai
3.Tangawizi iliyosagwa kijiko kimoja cha chai
4.Mafuta ya kupikia vijiko viwili vya chakula
5.Pilipili manga kijiko kimoja cha chai
6.Juisi ya limao nusu kikombe
7.Pilipili ya unga nyekundu kijiko kimoja cha chai
8.Tandoori masala au beef masala nusu kijiko cha chai
9.Vipande vya hoho vya shepu ya box
10.Vipande vya karoti vya shepu ya duara.
 
MAPISHI
1.Katakata nyama yako katika vipande vipande vidogo vya mishikaki
2.Chukua bakuli kubwa kisha mimina vitunguu saum,tangawizi,pilipilimanga,pilipili ya unga,tandoori masala kisha kamulia limao au ndimu kisha changanya vizuri.
3.Mimina vipande vya nyama katika hilo bakuli kisha changanya vizuri
4.Funika bakuli lako na acha kwa muda wa saa 1 hadi 3 au hifadhi kwenye fridge usiku kucha katika ubaridi wa wastani.
5.Loweka vijiti vya mishikaki katika maji kwa dakika 10.
6.Funua bakuli lako kisha chukua vijiti vya mishikaki kisha anza kuchomeka nyama, katikati ya kila nyama weka vipande vya karoti na hoho.
7.Weka mkaa katika jiko lako kisha weka wavu juu yake na anza kuchoma mishikaki yako hadi ibadilike rangi na kuwa kahawia.
Kama unatumia oven, weka mishikaki yako katika chombo cha kuokea kisha ingiza ndani ya oven, set moto katika digrii 140 iache kwa dakika 5, kisha fungua oven ipindue na iache kwa dakika 5 nyingine, hakikisha imebadirika rangi na kuwa kahawia.
Mishikaki yako ipo tayari kwa kula.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUPIKA MAANDAZI/MAHAMRI LAINI NA MATAMU SANA/how to make maanda...

JINSI YA KUKAANGA MIHOGO LAINI/ CASSAVA RECIPE

VYAKULA VINAVYOFAA KWA MTOTO KUANZIA MIEZI SITA MPAKA MIEZI TISA

  Ni wakati wa kuwa mbunifu sasa! Mtoto wako akiwa na miezi 6 mpaka 9 anakua na hamu ya kujaribu chakula kipya, na pengine kuanza kujifunza kutafuna pia. Sasa unahitaji kujifunza jinsi ya kuandaa milo ambayo itamvutia na kumshawishi mtoto kula vizuri.    JEE VYAKULA GANI NI VIZURI KUMWANZISHIA MTOTO MWENYE UMRI WA MIEZI SITA MPAKA TISA?   Wazazi na walezi wengi huuliza suali hili kwa lengo la kuhakikisha watoto wao wanapata chakula bora zaidi. Hakuna sheria wala kanuni katika suala hii. Watoto wote wako tofauti, kwa tabia zao maalumu za kupenda na kukataa vitu. Taarifa na mapishi yaliyomo kwenye sehemu hii ni mwongozo tu, kama mtoto wako hatopenda basi mwache kama wiki hivi halafu jaribu kumpa tena. Ladha kwake hubadilika kila mara kutokana na ukuaji wake wa haraka, hivyo kitu ambacho amekipenda leo huweza baada ya wiki akaanza kukikataa, na kinyume chake pia ni sawa. NB: kumbuka kutumia kanuni ya siku nnee kila unapomuanzishia mtoto chakula kipya (yani kumpa mtoto c...