Skip to main content

NJIA RAHISI YA KUTENGENEZA KEKI YA VANILLA

 NJIA RAHISI YA KUTENGENEZA KEKI YA VANILLA





-Fuatilia maelekezo yote bonyeza hapa


MAHITAJI
-Unga wa Ngano Vikombe 2
-Baking powder 1 kijiko cha chai
-Sukari kikombe 1
-Siagi kikombe 1 kidogo
-mayai 3
-Vanilla vijiko 2 vya chai
-Maziwa fresh
ukipenda

MAELEKEZO YA JINSI YA KUTENGENEZA KEKI
1.  kwenye bakuli kubwa,Chuja Unga,weka baking poda.

2.Blend sukari yako na blender au twanga sukari kidogo kidogo kufanya sukari iwe kama unga.

3.Kwenye bakuli nyingine, weka siagi na sukari uliyoponda ipige pige  na  mwiko mpaka siagi iwe smooth, kuelekea kama rangi nyeupe hivi(fanya kwa dk10 hv)

4.Baada ya hapo, piga mayai tia kwenye mchanganyiko wa siagi na sukari, kisha weka maziwa au fanya kidogo kidogo.

5.Sasa, chukua ule unga ulioandaa kwenye step ya 1, mimina kidogo kidogo kwenye mix ya mayai,siagi, sukari na maziwa.

6.Koroga mchanganyiko wako mpaka uwe kama uji mzito, koroga kwa kutumia mixer ya mkono au mixer ya umeme.(Angalia hapa)

JINSI YA KUOKA KEKI
-Andaa sufuria ya kuokea paka siagi chini

-Mimina mchanganyiko wako wa uji ukieneza kwenye angle zote za sufuria.

-Kama unatumia oven weka moto mdogo wa 350F

-Kama unatumia mkaa, basi hakikisha umeshawasha mkaa umekolea vizuri, Chukua mfuniko weka makaa ya moto juu ya mfuniko, bakisha mkaa kidogo sana,kisha weka sufuria yenye uji wa keki weka jikoni, funikia na mfuniko wenye makaa.

-Baada ya dk 15-30 utaskia harufu ya kuiva, funua mfuniko chomeka toothpick kwenye keki kuona kama imeiva toothpick ikitoka kavu bas keki imeiva epua.

-Weka kwenye sahani keki yako waweza kata vipande unavyotaka, tayari kuliwa.

NB: Usitumia baking soda au baking poda zilizokaa sana dukani au nyumbani mwisho miezi 6.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUPIKA MAANDAZI/MAHAMRI LAINI NA MATAMU SANA/how to make maanda...

JINSI YA KUKAANGA MIHOGO LAINI/ CASSAVA RECIPE

VYAKULA VINAVYOFAA KWA MTOTO KUANZIA MIEZI SITA MPAKA MIEZI TISA

  Ni wakati wa kuwa mbunifu sasa! Mtoto wako akiwa na miezi 6 mpaka 9 anakua na hamu ya kujaribu chakula kipya, na pengine kuanza kujifunza kutafuna pia. Sasa unahitaji kujifunza jinsi ya kuandaa milo ambayo itamvutia na kumshawishi mtoto kula vizuri.    JEE VYAKULA GANI NI VIZURI KUMWANZISHIA MTOTO MWENYE UMRI WA MIEZI SITA MPAKA TISA?   Wazazi na walezi wengi huuliza suali hili kwa lengo la kuhakikisha watoto wao wanapata chakula bora zaidi. Hakuna sheria wala kanuni katika suala hii. Watoto wote wako tofauti, kwa tabia zao maalumu za kupenda na kukataa vitu. Taarifa na mapishi yaliyomo kwenye sehemu hii ni mwongozo tu, kama mtoto wako hatopenda basi mwache kama wiki hivi halafu jaribu kumpa tena. Ladha kwake hubadilika kila mara kutokana na ukuaji wake wa haraka, hivyo kitu ambacho amekipenda leo huweza baada ya wiki akaanza kukikataa, na kinyume chake pia ni sawa. NB: kumbuka kutumia kanuni ya siku nnee kila unapomuanzishia mtoto chakula kipya (yani kumpa mtoto c...