Leo nitawaelezea jinsi ya kupika tambi tamu sana pamoja na nyama ya kusaga. Tambi zetu za leo ni tambiza bomba. Naam, Mapishi ya tambi yapo ya aina tofauti tofauti, kuanzia tambi za sukari na za chumvi ambazo kwamba aghlabu huandaliwa kwa nyama ya kusaga. Hata hivyo, wapo wengine wanaoandaa tambi kwa mchuzi wa viazi au hata mayai. Na leo nitawaelezea jinsi ya kupika tambi tamu sana za bomba pamoja na nyama ya kusaga.
MAHITAJI
1.Nyama ya kusaga robo kilo
2.Tambi za bomba robo kilo
3.Kitunguu maji kimoja cha wastani (kikate vipande vidogo dogo sana)
4.Nyanya kubwa 2
5.Kitunguu saum kijiko kimoja cha chakula
6.Tangawizi kijiko kimoja cha chakula
7.Pilipili manga ya unga kijiko kimoja cha chai
8.Tomato paste vijiko vitatu vya chakula
9.Chumvi kiasi
MAPISHI
1.Chukua sufuria weka jikoni kisha mimina mafuta ya kupikia
2.Mimina vipande vidogo dogo vya kitunguu maji kisha koroga vizuri
3.Mimina pilipili manga na koroga vizuri
4.Mimina kitunguu saum na tangawizi kisha koroga vizuri
4.Mimina rojo la nyanya na koroga vizuri
5.Nyanya ikichanganyika na viungo mimina nyama ya kusaga kisha changanya na viungo vyote.
6.Ongeza maji kidogo kisha acha nyama iivishwe na rojo la viungo, moto uwe wa wastani.Iache nyama kwa muda wa nusu saa.
7.Funua nyama kisha mimina tomato paste na koroga vizuri na funika acha kwa dakika 10.
8.Chemsha tambi za bomba hadi ziive vizuri ila yasiwe malaini sana.
9.Mimina tambi za bomba katika rosti la nyama ya kusaga na changanya vizuri kisha mimina chumvi na changanya vizuri
10.Funika kwa dakika 3
11.Tambi za bomba na nyama ya kusaga ipo tayari.
Andaa chai yako ya maziwa kisha kula pamoja na tambi za bomba na nyama ya kusaga.
Toa maoni niambie pishi gani ungependa kujua, follow kwa mapishi mengine zaidi.
Comments
Post a Comment