Leo nitawaelezea jinsi ya kupika tambi tamu sana pamoja na nyama ya kusaga. Tambi zetu za leo ni tambiza bomba. Naam, Mapishi ya tambi yapo ya aina tofauti tofauti, kuanzia tambi za sukari na za chumvi ambazo kwamba aghlabu huandaliwa kwa nyama ya kusaga. Hata hivyo, wapo wengine wanaoandaa tambi kwa mchuzi wa viazi au hata mayai. Na leo nitawaelezea jinsi ya kupika tambi tamu sana za bomba pamoja na nyama ya kusaga. MAHITAJI 1.Nyama ya kusaga robo kilo 2.Tambi za bomba robo kilo 3.Kitunguu maji kimoja cha wastani (kikate vipande vidogo dogo sana) 4.Nyanya kubwa 2 5.Kitunguu saum kijiko kimoja cha chakula 6.Tangawizi kijiko kimoja cha chakula 7.Pilipili manga ya unga kijiko kimoja cha chai 8.Tomato paste vijiko vitatu vya chakula 9.Chumvi kiasi MAPISHI 1.Chukua sufuria weka jikoni kisha mimina mafuta ya kupikia 2.Mimina vipande vidogo dogo vya kitunguu maji kisha koroga vizuri 3.Mimina pilipili manga na koroga vizuri 4.Mimina kitunguu saum na ...
Comments
Post a Comment