MISHIKAKI YA KUKU TIKKA Umeshawahi kula mishikaki ya kuku tikka? Jaribu leo mapishi yake MAHITAJI 1.Minofu ya kuku ya mapaja au ya kifua isiyo na mifupa kilo moja 2.Tangawizi iliyosagwa kijiko kimoja cha chakula 3.Kitunguu saum kilichosagwa kijiko kimoja cha chakula 4.Unga wa giligilani nusu kijiko cha chakula 5.Pilipili ya unga nusu kijiko cha chai 6.Unga wa mdalasini nusu kijiko cha cha 7.Pilipilimanga nusu kijiko cha chakula 8.Limao moja 9.Manjano kijiko kimoja cha chakula 10.Kitunguu maji kimoja 11.Majani ya giligilani 12.Unga wa binzari nyembamba kijiko kimoja cha chai 13.Mtindi nusu kikombe 14.Chumvi kiasi 15.Mafuta ya kupikia kiasi MAPISHI 1.Katakata minofu ya kuku ya kifua au mapaja kwa umbo la vibox 2.Chukua bakuli kubwa mimina vipande vya minofu ya kuku 3.Mimina viungo vyote vilivyotajwa na mafuta kiasi kisha changanya vizuri. 4.Chukua vyuma vya mishikaki au vijiti vya mishikaki kisha chomeka vipande vya minofu ya kuku 5.Andaa jiko lako la m...