Skip to main content

Posts

USAFI WA MIGUU

USAFI WA MIGUU:   Huu ni Usafi wa miguu ambao hautoi tu sumu mwilini mwako lakini utafanya miguu ipumzike, itandoa harufu mbaya ya miguu baada ya kukaa sana viatu na itaua kabisa bakteria mbaya na fungi mwilini.   MAHITAJI:   1. Beseni la kuoshea miguu lililojazwa maji ya uvuguvugu   2. Kijiko 1 kidogo cha maji ya limao   3. Kijiko 1 kidogo cha chumvi ya Epsom au baking Soda (Chochote kitakachopatikana)   4. ½ Kijiko cha mafuta ya mzaituni (olive)   5. Majani mawili au matatu ya muarubaini   6. Scrub ya miguu   7. Cream ya miguu yoyote inayopatikana au unaweza kutumia cream ya mwili pia.   JINSI YA KUANDAA:   Weka vitu vyote vilivyoainishwa (2-5) kwenye bakuli la maji ya moto. Hakikisha kuwa maji yana vuguvugu wa kutosha lakini hayapaswi kuwa moto sana yataunguza ngozi. Loweka miguu yako katika bakuli kwa dakika 15. Sugua miguu kidogo na scrub ya miguu kisha kausha na kitambaa. Paka moisturizer yako na uende kulala. Fanya h...

VYAKULA VINAVYOFAA KWA MTOTO KUANZIA MIEZI SITA MPAKA MIEZI TISA

  Ni wakati wa kuwa mbunifu sasa! Mtoto wako akiwa na miezi 6 mpaka 9 anakua na hamu ya kujaribu chakula kipya, na pengine kuanza kujifunza kutafuna pia. Sasa unahitaji kujifunza jinsi ya kuandaa milo ambayo itamvutia na kumshawishi mtoto kula vizuri.    JEE VYAKULA GANI NI VIZURI KUMWANZISHIA MTOTO MWENYE UMRI WA MIEZI SITA MPAKA TISA?   Wazazi na walezi wengi huuliza suali hili kwa lengo la kuhakikisha watoto wao wanapata chakula bora zaidi. Hakuna sheria wala kanuni katika suala hii. Watoto wote wako tofauti, kwa tabia zao maalumu za kupenda na kukataa vitu. Taarifa na mapishi yaliyomo kwenye sehemu hii ni mwongozo tu, kama mtoto wako hatopenda basi mwache kama wiki hivi halafu jaribu kumpa tena. Ladha kwake hubadilika kila mara kutokana na ukuaji wake wa haraka, hivyo kitu ambacho amekipenda leo huweza baada ya wiki akaanza kukikataa, na kinyume chake pia ni sawa. NB: kumbuka kutumia kanuni ya siku nnee kila unapomuanzishia mtoto chakula kipya (yani kumpa mtoto c...

FAIDA ZA OATS KWA MTOTO WAKO

  FAIDA ZA OATS KWA MTOTO WAKO Oats ni nzuri sana kiafya na imevutia sana katika zama za hivi karibuni. Hii ni kwa sababu ya faida za kiafya ambazo oats huleta kwenye meza.   INA NYUZI LISHE KWA WINGI SANA: Oats ina nyuzi lishe kwa wingi na wanga ambazo husaidia katika kurahisisha mfumo wa kumeng’enya chakula kufanya kazi vizuri. Zina aina ya nyuzi lishe ambazo zinayeyuka inayoitwa Beta-glucan ambayo husaidia kuongeza uwezo wa umeng’enyaji, kudhibiti shinikizo la damu na kudumisha viwango vya lehemu.   INA VITAMINI NA MADINI NYINGI: Oats ni chanzo bora cha magnesiamu, phosphorus, madini chuma, kalsiamu, folate, zinki, vitamini B1 & B5.Hii hufanya oats kuwa lishe bora na yenye utajiri mkubwa kwa mtoto wako!   INA KIASI KIKUBWA CHA PROTINI NA MAFUTA: Ungekuwa usijue kuwa oats kweli ina protini zaidi na mafuta kuliko nafaka nyengine nyingi. Hii ndio sababu ni nzuri kwa mtoto wako anayekua na kwa kweli inaweza kusaidia mtoto wako kupata uzito na afya ya ...

MASK ZA LIWA INAYOWAFANYA MAAJABU KWA MPAKO MMOJA TU

  Mask ya Maajabu ya Liwa Jeupe:   MOJA KATI YA MASK ZA LIWA INAYOWAFANYA MAAJABU KWA MPAKO MMOJA TU:  Hebu JAribu Ujionee Kuna mask ya liwa ambayo wengi wanaisifia na kuita ya ajabu kwa jinsi inavyofanya kazi haraka. Wengi wanaipenda sana hii pamoja na kua kuna aina nyingi sana za mchanganyiko wa liwa. Hii ina faida nyingi sana kwa ngozi ya uso! Kwa hivyo, ni zipi faida hizi ambazo ninazungumza? Tuende pamoja hapo chini:   FAIDA ZA ' MASK YA AJABU YA LIWA' 1. Inatoa mng’ao wa haraka kwenye ngozi na unaifanya ngozi ionekane nzuri kuliko kawaida. 2. Husaidia katika kuondoa ngozi iliyoharibika 3. Huacha ngozi ikionekana safi na nyororo 4. Inaipa ngozi unyevu vizuri sana 5. Inapunguza mafuta yoyote ya ziada yanayotengenezwa asili na ngozi 6. Inafanya ngozi kuwa laini na inayovutia 7. Ni toner nzuri ya asili kwa ngozi 8. Husaidia kuondoa chunusi, alama na mabaka meusi 9. inafaa kwa kila aina ya ngozi 10. Ni mask nzuri ya uso wa unaozeeka 11. Ina harufu nzuri Unapotu...

MAPISHI YA MISHIKAKI LAINI NA MITAMU SANA (JUICY MISHIKAKI)

Jinsi ya kupika mishkaki MAHITAJI 1.Nyama nusu kilo 2.Vitunguu saum vilivyosagwa kijiko kimoja cha chai 3.Tangawizi iliyosagwa kijiko kimoja cha chai 4.Mafuta ya kupikia vijiko viwili vya chakula 5.Pilipili manga kijiko kimoja cha chai 6.Juisi ya limao nusu kikombe 7.Pilipili ya unga nyekundu kijiko kimoja cha chai 8.Tandoori masala au beef masala nusu kijiko cha chai 9.Vipande vya hoho vya shepu ya box 10.Vipande vya karoti vya shepu ya duara.   MAPISHI 1.Katakata nyama yako katika vipande vipande vidogo vya mishikaki 2.Chukua bakuli kubwa kisha mimina vitunguu saum,tangawizi,pilipilimanga,pilipili ya unga,tandoori masala kisha kamulia limao au ndimu kisha changanya vizuri. 3.Mimina vipande vya nyama katika hilo bakuli kisha changanya vizuri 4.Funika bakuli lako na acha kwa muda wa saa 1 hadi 3 au hifadhi kwenye fridge usiku kucha katika ubaridi wa wastani. 5.Loweka vijiti vya mishikaki katika maji kwa dakika 10. 6.Funua bakuli lako kisha chukua vijiti vya mishikaki kisha anza kuc...

MAPISHI YA TAMBI ZA BOMBA NA NYAMA YA KUSAGA

 Leo nitawaelezea jinsi ya kupika tambi tamu sana pamoja na nyama ya kusaga. Tambi zetu za leo ni tambiza bomba. Naam, Mapishi ya tambi yapo ya aina tofauti tofauti, kuanzia tambi za sukari na za chumvi ambazo kwamba aghlabu huandaliwa kwa nyama ya kusaga. Hata hivyo, wapo wengine wanaoandaa tambi kwa mchuzi wa viazi au hata mayai. Na leo nitawaelezea jinsi ya kupika tambi tamu sana za bomba pamoja na nyama ya kusaga.     MAHITAJI   1.Nyama ya kusaga robo kilo 2.Tambi za bomba robo kilo 3.Kitunguu maji kimoja cha wastani (kikate vipande vidogo dogo sana) 4.Nyanya kubwa 2 5.Kitunguu saum kijiko kimoja cha chakula 6.Tangawizi kijiko kimoja cha chakula 7.Pilipili manga ya unga kijiko kimoja cha chai 8.Tomato paste vijiko vitatu vya chakula 9.Chumvi kiasi   MAPISHI   1.Chukua sufuria weka jikoni kisha mimina mafuta ya kupikia 2.Mimina vipande vidogo dogo vya kitunguu maji kisha koroga vizuri 3.Mimina pilipili manga na koroga vizuri 4.Mimina kitunguu saum na ...

7 LIPTRICKS YOU DON'T WANT TO MISS

 7 LIPTRICKS YOU DON'T WANT TO MISS WHEN BRUSHING TEETH, give lips a light brush with the toothbrush to remove dead skin. It also increases blood flow and lips lood flow and makes lips look full. MAKE LIP COLOUR LAST by applying lipstick, then press lips with tissue. Dust powder powder over the tissue with a puff or brush apply another layer of lipstick. COAT LIPS WITH PETROLEUM JELLY and leave for five minutes, then lightly scrub with a toothbrush or washcloth. EXFOLIATE LIPS WITH WITH FINE SALT AND OLIVE OIL or a lip scrub like Bliss Fabulips Sugar lip scrub then moisturise with lip balm. USE LIP LINER ONE SHADE LIGHTER than your lipstick. a darker shade makes lips look thinner and adds a years to your look. CREATE FULL LIPS by dabbing shimmer silver or gold lips gloss on the middle of your lower lip. LICK LIP BEFORE DRINKING; you will avoid leaving a mark on your drinking glass.