Skip to main content

NJIA SITA ZA KUNYWA MAJI YA MOTO ZINAZOTIBU MWILI WAKO

Kunywa kikombe kimoja cha maji ya moto kila asubuhi kinaweza kukutibu mwili wako kwa kusaidia umeng’enywaji wa chakula na kuzuia kuzeeka mapema kabla ya wakati.
Wengi wetu huianza asubuhi vyema kwa kikombe cha kawaha ya moto au chai ya moto kwa lengo la kuuchangamsha miili yetu baada ya kutoka kitandani. 




Na pale tunapokunywa maji, basi wengi wetu hupendelea kunywa ya baridi, lakini kwa mujibu wa watalaam wa afya wanatuambia kua tunafanya makosa kufanya hivyo. (kunywa maji baridi)
Mara nyingi unywaji wa maji moto au uvuguvugu, hususani nyakati za asubuhi, inasaidia kuiponya miili yetu na kuitibu pia,
kwa kusaidia kuongeza nguvu katika mmeng’enyo wa chakula ma kupunguza taka mwilini, taka ambazo zinaweza kuzuia kinga zetu kua katika hali yake nzuri ya mfumo sahihi na ambao tunauhitaji.


“matabibu wanasema na kushauri kunywa maji moto ama uvuguvugu nyakati za asubuhi, kila siku, sambamba na mchanyanyo wa maji ya limao, au chai ambayo haina madhara kwa mwili”. 


Utumiaji wa maji moto ama vuguvugu huongeza ukazwaji wa utumbo, ambapo husaidia uondoaji wa vitu visivyotakiwa. 
Tofauti na maji moto, utumiaji wa maji ya baridi yenyewe huzuia vitu muhimu ikiwemo madini ambayo hua si rafiki kwa mazingira hayo katika mfumo wa umeng’enywaji unapokula chakula.


Kwa wanywaji wa maji ya baridi, inashauriwa kutangulia kunywa maji hayo ya baridi dakika 20 kabla ya kula hata kama maji hayo yanatoka katika vyanzo vya asili vya maji. 
Wakati unywaji wa maji ya moto ama vuguvugu yanaweza yasiwe mazuri kwa ladha yanapokua mdomoni,


Hizi hapa zifuatazo ni sababu kwanini tunywe maji ya uvuguvugu,


1. Hurahisisha umeng’enywaji wa chakula,
Maji ya moto ama vuguvugu katika kikombe uamkapo asubuhi yanaweza kuusaidia mwili wako kutoa nje sumu katika mwili. 
Maji na vimiminika vingine husaidia kuvunja vunja chakula katika tumbo na kuweka mfumo wa chakula kuwa katika hali nzuri ndani ya mwili. Maji moto au vuguvugu husaidia kuweza kuvunja vunja chakula hicho kwa uharaka zaidi, na hivyo umeng’enywaji wa chakula kua mwepesi na wa haraka.
Unywaji wa maji ya baridi wakati ama baada ya mlo wako unaweza kusababisha kusaidia kugandishwa kwa mafuta ambayo unayapata kupitia chakula, na hivyo kusababisha mrundikano wa mafuta katika utumbo.
Uongezwaji wa barafu ili kutengeneza maji ya baridi hufanya kubadili mfumo halisi wa madini na virutubisho katika mwili ambavyo madini hayo ni muhimu katika kuuweka mfumo wa chakula katika hali ya afya, ambapo pia unaweza kufanya njia mbadala kwa kunywa chupa ya maji ya baridi sambamba na chupa ama glasi ya maji ya uvuguvu au moto ili kusaidia umeng’enywaji wa chakula, hususani baada ya kula chakula chako.





2. Husaidia kulainisha choo
Kwa pointi moja au nyingine, wengi wetu tunakabiliwa na vidonda hususani matatizo ya tumbo ambapo hua na choo kidogo au kukosa kabisa haja kubwa.
Vile vile ugumu wa haja uendapo msalani wakati wa kukitoa, husababisha kuchanika au kuchubuka katika sehemu ya kupitia haja kubwa, 
Haya yote yanaletwa na ukosefu wa maji mwilini. 
Unywaji wa maji moto au vuguvugu nyakati za asubuhi wakati tumbo likiwa halina kitu unaweza kusaidia utumbo mpana kusukuma uchafu/ kinyesi vizyri na kusaidia kuwa na choo laini wakati wa uvunjwaji wa chakula na hata usafirishwaji wake hua mzuri kupita utumbo. 
Hivyo uchangamshwaji wa utumbo na maji moto husaidia kuurudisha mwili katika ufanyaji wake mzuri na wakawaida wa kazi vyema.


3. Huondoa maumivu
Maji ya moto au vuguvugu, tukizingatia ni maji asilia ambayo wengi wetu katika majumba hutumia, husaidia kuondoa maumivu ya tumbo la hedhi kwa wakina mama na maumivu ya kichwa.
Umotomoto toka kwenye maji moto huweza kua na athari chanya katika misuli ya tumbo, ambapo huweza kusaidia kuondoa papo kwa papo makazo na misuli kujinyoosha. 
Kwa mujibu wa Healthline, wanasema maji moto au vuguvugu ni mazuri kwa maumivu, ambapo kimiminika hicho cha moto huongeza mzunguko wa damu kwenye ngozi na kusaidia kushusha maumivu ya misuli.


4. Husaidia kupunguza uzito
Kama uko katika mlo wako, unywaji wa maji nyakati za asubuhi basi unaweza kukusaidia katika kupunguza uzito. 
Maji moto ama uvuguvugu husaidia kuongeza joto la mwili, ambapo huongeza metabolic/ kiwango cha ufanisi wa kazi katika mwili. 
Kadri kiwango cha ufanisi wa kazi katika mwili kinapoongezeka huuruhusu mwili kuchoma kalori nyingi katika mwili. 
Hivyo husaidia figo na gastro intestinal kufanya kazi zake vizuri mwilini.
“madaktari wanashauri kua unywaji wa maji moto nyakati za asubuhi, kila siku, pamoja na limao ndani yake, au chai huondoa vitu hatari mwilini”.
Unywaji wa glasi kadhaa za maji moto au vuguvugu na limao ndani yake husaidia kuvunjavuja tisu za mafuta katika mwili na husaidia mmeng’enyo wa chakula.




5. Kuboresha mzunguko wa damu
Mrundikano wa mafuta katika mwili huondolewa wakati wa unywaji wa maji ya moto. 
Hii husaidia kuondoa sumu ambazo hua zimezunguka katika miili yetu kwa kufanikisha mzunguko wa damu.


6. Hupunguza hatari ya kuzeeka mapema
Hii inaweza kuzuilika kwa kunywa maji moto ama vuguvugu, upatikanaji wa sumu katika mwili hupelekea kuzeeka mapema na kwa haraka, lakini maji moto ama vuguvugu YAnaweza kusaidia kusafisha mwili kwa kutoa sumu mwilini, hata hivyo pia kuirekebisha ngozi kwa kuoneza SelI mpya maeneo ya ngozi. 
Medical Daily linasema kua “wanawake siku zote hunufaika kwa sababu wanakua na homoni nyingi zaidi ambazo huhusika na maji moto,”
Kuweza kua ama kuongeza uimara wa afya yako kupitia unywaji wa maji moto ama vuguvugu, kunywa kila siku asubuhi maji pekee au yaliyochanganywa na limao kwa kuyapa ladha. 
Wanywaji wa maji vuguvugu au moto kwa, kadiri wanavyokunywa maji hayo wanaweza kua wanaangamiza tisu za mdomoni na hata maeneo ya koromeo. 
Baada ya kuunguzwa na maji hayo ya moto,
Basi huna budi kuyaacha yapoe kidogo kabla ya kuanza kuyatumia kwa kuyanywa.
Vile vile inashauriwa “ kila mara umuone daktari kwa maelezo kabla ya kuanza kunywa maji hayo ya moto, kama utakua katika matumizi mengine ya dawa, ambazo zinaweza kuleta madhara katika ufanisi wa dawa husika.

Comments

Popular posts from this blog

NJIA ASILIA YA KUINUA MATITI YALIYOANGUKA,KUPUNGUZA MATITI MAKUBWA NA KUJAZA YALIYOSINYAA

kiukweli matiti yaliyolala humkosesha mrembo raha kuna njia tofauti zaa kuyainua matiti.  K wa wakina dada na mama ambao maziwa yenu yanawakela hii ndo dawa yake fanya kwa wiki mara mbili utayafurahia maziwa yako. Mahitaji olive oil au coconut oil vitamin E oil ndizi mbivu yai la kienyeji juice ya kitunguu maji 1tbsp Njia ya kwanza safisha maziwa yako vizuri kisha chukua ute wa yai upige kwa kijiko ulainike ongeza juice ya kitunguu maji paka matiti yako acha ikauke Njia YA PILI kama matiti yako ni makubwa fanya njia hii ya pili kama sio makubwa iache tangawizi 1tsp limao1tsp changanya mchanganyiko huo kisha paka matiti yako kwa dkk tano iache ikauke usioshe twende hatua ya tatu kama titi lako limesinyaa baada ya kumaliza hatua au njia ya kwanza fanya hii chukua kiazi mviringo kikwangue na kikwaruzo pakaa matiti yako acha ikauke usioshe. ...

MAPISHI YA MISHIKAKI LAINI NA MITAMU SANA (JUICY MISHIKAKI)

Jinsi ya kupika mishkaki MAHITAJI 1.Nyama nusu kilo 2.Vitunguu saum vilivyosagwa kijiko kimoja cha chai 3.Tangawizi iliyosagwa kijiko kimoja cha chai 4.Mafuta ya kupikia vijiko viwili vya chakula 5.Pilipili manga kijiko kimoja cha chai 6.Juisi ya limao nusu kikombe 7.Pilipili ya unga nyekundu kijiko kimoja cha chai 8.Tandoori masala au beef masala nusu kijiko cha chai 9.Vipande vya hoho vya shepu ya box 10.Vipande vya karoti vya shepu ya duara.   MAPISHI 1.Katakata nyama yako katika vipande vipande vidogo vya mishikaki 2.Chukua bakuli kubwa kisha mimina vitunguu saum,tangawizi,pilipilimanga,pilipili ya unga,tandoori masala kisha kamulia limao au ndimu kisha changanya vizuri. 3.Mimina vipande vya nyama katika hilo bakuli kisha changanya vizuri 4.Funika bakuli lako na acha kwa muda wa saa 1 hadi 3 au hifadhi kwenye fridge usiku kucha katika ubaridi wa wastani. 5.Loweka vijiti vya mishikaki katika maji kwa dakika 10. 6.Funua bakuli lako kisha chukua vijiti vya mishikaki kisha anza kuc...

JINSI YA KUKUZA NYWELE HARAKA

Wanawake wa kiafrika hua wana nywele fupi na ngumu, yaani hii ni asili yao tofauti na wanawake wa rangi zingine duniani kama wachina, wazungu, wajapani, wafilipino na kadhalika.. nywele za waafrika mara nyingi haziwi ndefu lakini kutokana na kubadilika kwa teknolojia, sasa hivi kuna uwezekano wa kukuza nywele zao kwa kufuata kanuni kadhaa za urembo na afya kama ifuatavyo. Tumia hina na Yai Kila baada ya siku nne uwe na utaratibu wa kupakaa mchanganyiko wa hina na mayai, iwe na paste nzito kiasi, upake katika mizizi ya nywele, ukimaliza kupaka nywele zifunike kwa mfuko maalum ili zipate joto kwa muda wa masaa mawili, Baada ya hapo zioshe kwa maji na shampoo, lakini maji yawe ya baridi yasiwe ya motooo au vuguvugu, yani yawe maji ya kawaida. Baada ya kuziosha zikaushe kwa taulo Zifahamu aina ya  nywele zako kitu cha kwanza kujua ni kizifahamu nywele zako, kuna watu wanakaa na nywele bila kujua nwele zake ni za iana gani,Jinsi ya kujua aina ya nywele zako , chomoa nyw...