Ukija kwenye fresh juice ya ukwaju ni nzuri zaidi kwa afya. . Unaweza tengeneza ya ukwaju mtupu bila kuchanganya na tunda jengine, ila leo tutachanganya na tunda la pesheni.
MAHITAJI
- Ukwaju mbivu kikombe 1
- Mapeshen 5
- Ndimu (za kijani ) 2
- Suakari unavyopenda
NJIA
- Roweka ukwaju kwa dakika 10 mpaka 15 ili uwe mlaini kusagika,
- Usage na blender vizuri, kama una kokwa usiusage moja kwa moja , saga kwa sekunde 2 , zima, fanya kama mara 4 au 5 au mpaka uone umesagika,
- Au unaweza kuufikicha kwa mkono tu
- Then uchuje kwa chujio
- Kwenye blender tia ile juice ya ukwaju na utie mapeshen yote(kokwa zake) uendelee kusaga mpaka mapeshen yasagike, kata ndimu vipande vidogo vidogo tia saga tena kwa sekunde 3 tu, ndimu zisisagike sana.
- Ichuje tena, hakikisha unatumia chujio au chungio nyembamba ili kuzuwiya mabaki ya peshen yasipenye,
- Iangalie /ionje juice kama ni kali sana itie maji kiasi, kama ipo sawa itie sukari unavyopenda, weka kwenye fridge au weka barafu na enjoy. Inapendeza sukari ukasagia blender pia.
PILAU YA SAMAKI
Samaki amemkaangwa ila wakwako wewe unaweza kumkausha au kumchoma ukipenda
Tayarisha samaki wako wa kukaanga au kukausha au kuchoma then endelea na hatua nyengiene hapo chini.
MAHITAJI
- Mchele nusu kg
- Viazi 2 (2 potatoes )
- Kitunguu maji 1 kikubwa (onion)
- Pilipili boga (capsicum ) kiasi. .imetumika red kidogo na green kidogo
- Bizari nyembamba 1 tbsp (cumin seed)
- Pilipili manga 1 tsp (black pepper)
- Bay leaves 3
- Mdalasini vipande 3 (cinnamon )
- Iliki chembe 4 (cardamom )
- Karafuu kavu chembe 4 (cloves )
- Mafuta ya kupikia 5 tbsp
- Kidonge cha supu 1 (maggi cube )/vegetable maggi
- Kitunguu saum 1 tbsp(garlic)
- Tangawizi mbichi 1 tbsp (ginger)
NJIA
- Roweka mchele kwa dakika 10 au zaidi,
- Chukua bizari nzima, Pilipili manga, mdalasini, iliki, karafuu na bay leaves zipashe moto kwa sufuria au pan kwa dakika 2, then zisage zote kwa pamoja ziwe unga,
- Teleka sufuria kwenye moto weka mafuta, yakipata anza kukaanga viazi, vikikaribia kuwiva weka kitunguu maji, wacha kiwive kiasi weka pilipili boga , kitunguu saum na tangawizi,
- koroga kiasi wacha kwa dakika 1 au 2, tia kidonge cha supu pamoja na spices ulizozisaga, koroga kidogo tu, weka maji yamoto kiasi ya kuwivisha wali , usiweke maji mengi, afadhali uweke kidogo badae ukiona hayajatosha uengeze, ukiongeza maji wakati ushaweka mchele lazima yawe yamoto otherwise yanaweza kuharibu muonekano wa wali, )
- Maji yakichemka angalia chumvi kama ipo OK weka mchele koroga kidogo tu, punguza moto funika wacha uchemke kidogo kidogo mpaka unakauka, then funua koroga tena kidogo kuugeuza ukiona umeshawiva pambia au weka moto mdogo juu weka wale samaki uliowapika ili watie harufu wali na ufunike kwa dakika 15 mpaka 20 au mpaka uwive.
- Baada ya hapo funua mtoe samaki, uchanganye taratibu bila kuuvuruga na ENJOY.
- Kiwango cha maji bcoz inategemea na mchele unaotumia, *unaweza kuongeza spices unazopenda.
Unaweza kula chakula chako na kinywaji chako cha juice ya ukwaju na pesheni, na kufurahia mlo wako wa mchana.
Comments
Post a Comment