Hivi karibuni watu wengi tumekuwa tukiangalia ubora wa simu ndo tuipe maksi, kama ukiona simu yako ina Megapixels 20 basi utafurahi, lakini ubora tu wa kamera ya simu haitoshi kukupa picha nzuri kama tunavyotarajia, kwa upigaji wa picha nzuri inahitaji ujuaji wa utumiaji teknohama iliyounda mfumo wa kamera yako ili ikupe picha nzuri.
Hizi ni dondoo chache za kujua ili simu yako ikupe picha bomba
- Kujua jinsi ya kuweka “Auto mode”
“Auto mode” ni mfumo ambayo kamera huchagua marekebisho yenyewe kutokana na sehemu uliyopo kama kuna mwanga hafifu, hii itakusaidia sana kupiga picha yenye viwango
- Kufanya marekebisho ambayo yamewekwa “Override the Defaults”
Simu nyingi za kisasa zinakuja na mipango “settings” moja kwa moja, lakini mara nyingi hushindwa kutambua ni mipango gani iweke kama ukiwa ndani au kukiwa na mawingu, ukijua kubadilisha kutokana sehem ulipo, utaishaidia sana simu yako kupata picha nzuri.
- Rekebisha “Edit”
Hii ni sehem ambayo watu wengi wanaifanya siku hizi, baada ya kupiga picha unaweza ukairekebisha kama kuongeza au kuunguza mwanga, kuikata, kuongeza rangi na kadhalika, lakini kujua ni mfumo “Application” gani nzuri kwa kufanya hivyo itasaidia sana kuifanya picha yako iwe nzuri kutokana na vitu ambavyo inavyo. Mfano wa mifumo mizuri ni kama Photo Grid, Cymera, Instagram, Aviari n.k
- Angalia Aina nyingine
Sio lazima utumia kamera ambayo imekuja na simu, unaeza ukaingia kwenye mtandao kama play store na kuangalia kamera amabayo itakufaa Zaidi ili ikupe majibu mazuri zaidi.
- Usikuze “Don’t Zoom”
Simu nyingi zina uwezo wa kukuza au kuvuta kitu ambacho ni cha mbali, lakini haina mfumo madhubuti wa kufanya hivyo, kwa hiyo inachofanya ni kukuza na kukata picha “Zoom and Crop” kabla haijaisave, hii ndio maana inaharibu uzuri wa picha yako .
Mwisho, vidokezo vya ziada ni kwamba hakikisha simu yako umeiweka katika chaguo la juu kabisa la picha inayopiga “Resolution” simu ngine zina uwezo mkubwa sana kama 1080p itakusaidia kupata picha nzuri sana, pia wakati wa kurekodi video tumia DDR au 60 frames per seconds kwa video nzuri, lakini kumbuka unavyopandisha machaguo ndio picha inavyohitaji nafasi kwenye simu yako
Comments
Post a Comment