Jinsi ya kupika mishkaki MAHITAJI 1.Nyama nusu kilo 2.Vitunguu saum vilivyosagwa kijiko kimoja cha chai 3.Tangawizi iliyosagwa kijiko kimoja cha chai 4.Mafuta ya kupikia vijiko viwili vya chakula 5.Pilipili manga kijiko kimoja cha chai 6.Juisi ya limao nusu kikombe 7.Pilipili ya unga nyekundu kijiko kimoja cha chai 8.Tandoori masala au beef masala nusu kijiko cha chai 9.Vipande vya hoho vya shepu ya box 10.Vipande vya karoti vya shepu ya duara. MAPISHI 1.Katakata nyama yako katika vipande vipande vidogo vya mishikaki 2.Chukua bakuli kubwa kisha mimina vitunguu saum,tangawizi,pilipilimanga,pilipili ya unga,tandoori masala kisha kamulia limao au ndimu kisha changanya vizuri. 3.Mimina vipande vya nyama katika hilo bakuli kisha changanya vizuri 4.Funika bakuli lako na acha kwa muda wa saa 1 hadi 3 au hifadhi kwenye fridge usiku kucha katika ubaridi wa wastani. 5.Loweka vijiti vya mishikaki katika maji kwa dakika 10. 6.Funua bakuli lako kisha chukua vijiti vya mishikaki kisha anza kuc...
Comments
Post a Comment