Wanawake wa kiafrika hua wana nywele fupi na ngumu, yaani hii ni asili yao tofauti na wanawake wa rangi zingine duniani kama wachina, wazungu, wajapani, wafilipino na kadhalika.. nywele za waafrika mara nyingi haziwi ndefu lakini kutokana na kubadilika kwa teknolojia, sasa hivi kuna uwezekano wa kukuza nywele zao kwa kufuata kanuni kadhaa za urembo na afya kama ifuatavyo.
Tumia hina na Yai
Kila baada ya siku nne uwe na utaratibu wa kupakaa mchanganyiko wa hina na mayai, iwe na paste nzito kiasi, upake katika mizizi ya nywele, ukimaliza kupaka nywele zifunike kwa mfuko maalum ili zipate joto kwa muda wa masaa mawili,
Baada ya hapo zioshe kwa maji na shampoo, lakini maji yawe ya baridi yasiwe ya motooo au vuguvugu, yani yawe maji ya kawaida. Baada ya kuziosha zikaushe kwa taulo
Baada ya hapo zioshe kwa maji na shampoo, lakini maji yawe ya baridi yasiwe ya motooo au vuguvugu, yani yawe maji ya kawaida. Baada ya kuziosha zikaushe kwa taulo
Zifahamu aina ya nywele zako
kitu cha kwanza kujua ni kizifahamu nywele zako, kuna watu wanakaa na nywele bila kujua nwele zake ni za iana gani,Jinsi ya kujua aina ya nywele zako , chomoa nywele moja katika kichwa chako na uhakikishe imetoka na kale kamzizi kanakokuwa na rangi ya weupe ivi, kisha dumbukiza unywele huo kwenye glasi yenye maji na angalia kama unywele uo unaleta matokeo gani,kama itazama mara moja na haitanyanyuka tena basi jua nywele yako inanyonya unyevu kwa haraka ivyo inaitaji kuwa na unyevu unyevu na kama .
Linda umyevu wa nywele zako.
kama ilivyo kiu kwa binadamu, ndivyo hivyo nywele huitaji maji, kwaio kipindi unapokuwa unaosha nywele zako kabla ya kuzipaka mafuta ya kulinda nywele zako jitahidi kuwa una fanya deep condition ili kuzifanya zibaki na unyevu .
Usafi wa ngozi na nywele zenyewe pia.
Kuna watu wanasema kuwa nywele zikioshwa mara kwa mara zinadumaa, lakini ulishawahi kujiuza endapo wewe utakaa bila kuoga.Nywele zinahitajika kuwa safi na ngozi yake pia ili kuifanya ngozi kufunguka na sio kufungwana ule uchafu wa mafuta.Matundu yanapokuwa wazi ndio ufanya nywele kuweza kujitokeza ivyo jitahidi kuosha nwele na kuhakikisha kuwa ngozi yako ni safi.
Chagua Mafuta bora ya kupaka
Jitahidi kuchagua mafuta mazuri kwa ajili ya nywele zako.sio kila mafuta yanafaa kupaka katika nywele zako ingawa mafuta ya nazi ni mazuri zaidi au mafuta ya olive.kitu kizuri ni kuzijua nywele zako kwanza ndipo utaweza kujua pia bidhaa bora ya mafuta kwa ajili ya nywele.Ukishindwa ni bora kuonana na wataalamu wa mambo ya urembo.
Epuka kuzisumbua nywele kila wakati.
Ni vizuri kuwa unachana nywele kwa muoekano mzuri wa sura yako na nwele pia, lakini kitendo icho ufanya nywele kuwa zinapuputika sana,jitahidi kuwa unazisuka ili kuzifanya zikue pia.Kuchana chana nywel ni kuzisumbua.
Inawezekana inakuwa ni ngumu kutambua nywele zake zinahitaji mafuta ya aina gani, au bidhaa gani ni bora zaidi kwa nywele zako, ni vizuri pia kuonana na wataalamu ili kuzisaidia nywele zako.
Comments
Post a Comment