Ni wakati wa kuwa mbunifu sasa! Mtoto wako akiwa na miezi 6 mpaka 9 anakua na hamu ya kujaribu chakula kipya, na pengine kuanza kujifunza kutafuna pia. Sasa unahitaji kujifunza jinsi ya kuandaa milo ambayo itamvutia na kumshawishi mtoto kula vizuri. JEE VYAKULA GANI NI VIZURI KUMWANZISHIA MTOTO MWENYE UMRI WA MIEZI SITA MPAKA TISA? Wazazi na walezi wengi huuliza suali hili kwa lengo la kuhakikisha watoto wao wanapata chakula bora zaidi. Hakuna sheria wala kanuni katika suala hii. Watoto wote wako tofauti, kwa tabia zao maalumu za kupenda na kukataa vitu. Taarifa na mapishi yaliyomo kwenye sehemu hii ni mwongozo tu, kama mtoto wako hatopenda basi mwache kama wiki hivi halafu jaribu kumpa tena. Ladha kwake hubadilika kila mara kutokana na ukuaji wake wa haraka, hivyo kitu ambacho amekipenda leo huweza baada ya wiki akaanza kukikataa, na kinyume chake pia ni sawa. NB: kumbuka kutumia kanuni ya siku nnee kila unapomuanzishia mtoto chakula kipya (yani kumpa mtoto c...
Comments
Post a Comment